Polepole aitwa polisi kutoa ushahidi wa tuhuma anazotoa

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 hours ago
rickmedia: polepole-aitwa-polisi-kutoa-ushahidi-tuhuma-anazotoa-182-rickmedia

Jeshi la Polisi limemwelekeza aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole afike katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) atoe maelezo na ushahidi kuhusiana na tuhuma ambazo amekuwa akizitoa kupitia mitandao ya kijamii.

Jeshi hilo limesema mbali na kukusanya ushahidi, limekuwa likifanya jitihada za kumpata ili aweze kutoa maelezo na vielelezo vitakavyothibitisha tuhuma hizo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.