Ofisi ya Mwendesha Mashtaka imesema haioni sababu za kumshtaki Rais Cyril Ramaphosa kutokana na Wizi wa Fedha uliodaiwa kufanywa na waliokuwa Wafanyakazi wake kwenye Shamba lake la Mifugo huko Limpopo.
Mkurugenzi wa Mashtaka amesema “Uamuzi wa kutomshtaki ulichukuliwa baada ya tathmini ya kina ya ushahidi wote uliowasilishwa. Kulingana na ushahidi uliopo, hakukuwa na sababu za kuridhisha za kufungua mashitaka”.
Kashfa hiyo iliyowekwa wazi na mmoja wa Maafisa wa Usalama wa Taifa ilimweka matatani Ramaphosa kiasi cha kukaribia kumwondoa madarakani ikidaiwa alikuwa akificha Fedha nyingi katika nyumba zilizopo shambani hapo, ingawa yeye alidai ni kiasi kidogo kilichokuwepo.