Rubani wa Shirika la Ndege la Uturuki, aliyefahamika kwa jina la İlçehin Pehlivan (59) ameripotiwa kufariki wakati Ndege ikiwa angani na kusababisha Msaidizi wake kuishusha Ndege kwa dharura Jijini New York.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Shirika hilo, Yahya Üstün amesema Rubani alizimia na hivyo kupewa huduma ya kwanza lakini alipoteza maisha na hivyo Msaidizi wake akaendesha Ndege na kutua ikiwa salama na Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F. Kennedy.
Taarifa imeeleza zaidi kuwa sababu za kifo cha Rubani huyo aliyefanya kazi na Turkish Airlines tangu mwaka 2007 bado hakijafahamika, pia, rekodi za uchunguzi zimeonesha Machi 8, 2024 alifanyiwa Vipimo vya Afya na hakukutwa na changamoto yoyote.