Serikali imepiga marufuku mijadala ya Wananchi kuhusu hali ya kiafya na mahali alipo Rais Paul Biya (91) ikidaiwa mijadala hiyo inahatarisha Usalama wa Nchi.
Hali hiyo inafuatia kutoonekana hadharani kwa Kiongozi huyo ambaye mara ya mwisho alihudhuria Mkutano wa Ushirika kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika Beijing Septemba 8, 2024.
Magavana wameagizwa kuunda vikosi vya kufuatilia na kurekodi vipindi na mijadala inayohusu Afya ya Biya inayofanyika kwa siri au hadharani na kuzitaarifu mamlaka.
Ikumbukwe, Biya ndiye Rais mzee zaidi duniani ambaye bado yuko madarakani akiwa ni Rais wa awamu ya pili na aliyeitawala Cameroon tangu Novemba 6, 1982.