Mwanahabari mkongwe wa Uganda, Shaka Ssali, amefariki dunia Machi 27, 2025, akiwa na umri wa miaka 71.
Ssali alipata umaarufu mkubwa katika kipindi cha "Straight Talk Africa" kinachorushwa na shirika la habari la nchini Marekani la Voice of America (VOA), ambacho alikiendesha kwa zaidi ya miongo miwili.
Katika kipindi cha utangazaji, Ssali alifanya mahojiano na viongozi mbalimbali wa Afrika, wachambuzi, na raia wa kawaida, akichochea mijadala kuhusu demokrasia, utawala bora na maendeleo barani Afrika.
Mwanabari huyo alivuma zaidi na kauli yake maarufu "I'm profoundly honored and exceedingly humbled" iliyotambulika na wengi kama alama ya kipindi chake.
Septemba 2024, Ssali alitunukiwa Tuzo ya Mafanikio ya Maisha na Jumuiya ya Waganda wa Amerika Kaskazini (UNAA), ikitambua mchango wake mkubwa katika tasnia ya habari barani Afrika.