Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Uganda limesema Maambukizi ya Mpox Nchini humo yameongezeka na kufikia visa 800, kutoka visa 495 vilivyoripotiwa kufikia Novemba 20, 2024, huku vifo vikiwa vinne.
Waziri wa Afya, Dkt Jane Ruth Aceng, amesema Serikali inaongeza juhudi za kukabiliana na kuongezeka kwa visa hivyo na kuwataka Watu kujilinda zaidi kwa kuepuka kugusana na Mtu mwenye Maambukizi.
Kwa mujibu wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (CDC), Mipira ya Plastiki (Kondomu) haizuii maambukizi ya Mpox kwa asilimia 100, kwasababu ingawa Kondomu zinaweza kutoa ulinzi kwa sehemu ya Mwili iliyofunikwa, vipele vinaweza kutokea kwenye sehemu nyingine za Mwili.