Loading...

Fomu ya kugombea Urais DR.Congo ni Sh.150 Milioni, 25 wajitokeza kuchukua

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

7 months ago
rickmedia: fomu-kugombea-urais-drcongo-sh150-milioni-wajitokeza-kuchukua-252-rickmedia

Wakati wagombea urais wa Tanzania wakitoa Sh5 milioni kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano, kwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wagombea Urais wanatakiwa kuonyesha risiti ya malipo ya faranga za Congo milioni 160, sawa na zaidi ya Sh150.3 Milioni kama ada zisizorejeshwa kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (CENI).

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), kiasi hicho kimepunguzwa kutoka Dola 100,000 sawa na zaidi ya Sh250.5 Milioni katika uchaguzi uliopita wa 2018.

Mpaka sasa wagombea 25 wameshajitokeza akiwamo Rais wa sasa Felix Tshisekedi akipambana na mpinzani wake wa karibu, Martin Fayulu ambaye katika uchaguzi wa mwaka 2018 ilidaiwa alishinda ingawa si aliyetangazwa.