Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Atoa siku 21 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ileje, Nuru Kindamba Kupitia majina ya watuhumiwa wa wizi wa vifaa vya ujenzi wa Zahanat

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

10 months ago
rickmedia: katibu-tawala-mkoa-songwe-atoa-siku-kwa-mkurugenzi-mtendaji-halmashauri-wilaya-ileje-319-rickmedia

Happiness Seneda ambaye ni katibu Tawala Mkoa wa Songwe Atoa siku 21 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ileje, Nuru Kindamba Kupitia majina ya watuhumiwa wa wizi wa vifaa vya ujenzi wa Zahanati ya Mtima na shinji.

Pia amemuagiza ampe sababu za kushindwa kusimamia Miradi ya Zahanati hizo mbili ambazo zipo katika halmashauri hiyo,Seneda ameyasema hayo Leo jumatano 6 December 2023 wakati akikagua Zahanati hizo na kubaini mapungufu ya Usimamizi katika Miradi hiyo zikiwemo na taarifa zenye Mkanganyiko.

Seneda anaeleza katika Zahanati hizo ambazo serikali ilitoa sh million 50 huku wananchi walichangia million 20 za ujenzi wa Boma na Matundu Mapya ya Vyoo,alibaini upotevu Vifaa na marumaru 41.