Kiongozi wa Kijeshi, Mahamat Idriss Deby Itno (39) ametangaza kuwania Urais katika #Uchaguzi utakaofanyika Mei 6, ikiwa ni Siku chache tangu mpinzani wake Mkuu kuuawa.
Deby Itno alichukua Madaraka Mwaka 2021 ambapo Utawala wa Kijeshi ulimtangaza kuwa Rais wa Mpito na kuahidi kurejesha Utawala wa Kiraia katika kipindi cha Miezi 18 lakini aliongeza kipindi cha mpito kwa Miaka miwili.
Mpinzani Mkuu wa Deby, Yaya Dillo Djeru aliuawa Februari 28, 2024, huku kukiwa na ripoti za Upinzani kukandamizwa Nchini huko.