Majimbo Ya marekani Yamfungulia Trump Kesi

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

17 hours ago
rickmedia: majimbo-marekani-yamfungulia-trump-kesi-88-rickmedia

Zaidi ya majimbo 20 yamewasilisha kesi dhidi ya utawala wa Rais wa Marekani #DonaldTrump kuhusu mabilioni ya dola ya ufadhili uliositishwa ambao ulikuwa umelengwa kwa ajili ya mipango ya baada ya shule na ya majira ya kiangazi.

#AidenCazares anawakilisha watoto na vijana wapatao milioni 1.4 kote nchini Marekani ambao wamefaidika na mipango ya fedha ya baada ya shule na majira ya kiangazi kupitia mashirika kama Boys & Girls Clubs, YMCA, na shule za umma, iliyofadhiliwa na walipa kodi wa serikali kuu.

Bunge la Marekani lilitenga fedha hizi kwa ajili ya kutoa msaada wa kitaaluma, shughuli za kukuza vipaji, na huduma ya malezi kwa familia zenye kipato cha chini, utawala wa #Trump hivi karibuni umesitisha ufadhili huo.

Siku ya jana Jumatatu, zaidi ya majimbo 20 yanayoongozwa na Wademokrasia yalichukua hatua kwa kuwasilisha kesi ili kulazimisha utawala wa #Trump kuachilia fedha hizo. Kesi hiyo, inayoongozwa na jimbo la California, inadai kuwa kuzizuia fedha hizo ni kinyume na Katiba na sheria mbalimbali za serikali ya shirikisho.

Iwapo fedha hizi hazitatolewa haraka, familia nyingi zenye kipato cha chini zinaweza kupoteza huduma za programu za baada ya shule, jambo linaloleta wasiwasi mkubwa hasa shule nyingi zinapotarajiwa kufunguliwa tena mwishoni mwa Julai na mapema Agosti.