Rais wa Malawi azuia viongozi kusafiri nj'e ya Nchi ili kubana matumizi

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

3 weeks ago
rickmedia: rais-malawi-azuia-viongozi-kusafiri-nje-nchi-ili-kubana-matumizi-265-rickmedia

Rais Lazarus Chakwera amesitisha mara moja safari zote za Kimataifa zinazomuhusisha yeye na Maafisa wote wa Serikali huku akiwaagiza Mawaziri walioko nje ya Nchi kwa sasa kurejea haraka.

Pia, ameweka vikwazo vya Safari za ndani ya Nchi na kupunguza kwa nusu ya mgawo wa Mafuta kwa Mawaziri na Maafisa Wakuu wa Serikali, uamuzi utakaotumika hadi mwisho wa Mwaka wa Fedha ujao (Machi 2024).

Aidha, amemtaka Waziri wa Fedha kuweka masharti ya nyongeza ya Mishahara kwa Watumishi wote wa Umma katika mapitio ya Bajeti ya Mwaka 2024/25 pamoja na kupunguzwa kwa Kodi ya Kipato (PAYE) kwa Wafanyakazi akieleza Mapato yao yamepoteza thamani kutokana na Mfumuko wa Bei.

Hatua ya Rais Chakwera inakuja baada ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kuidhinisha mkopo wa Miaka 4 wa Tsh. Bilioni 435.5 Siku chache tangu Benki Kuu kutangaza thamani ya Sarafu ya Malawi imeshuka kwa 44%.