Rais Tshisekedi na Rais Kagame wakutana Qatar kujadili mzozo wa M23

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 weeks ago
rickmedia: rais-tshisekedi-rais-kagame-wakutana-qatar-kujadili-mzozo-m23-755-rickmedia

Rais wa DRC, Félix Tshisekedi na Rais wa Rwanda, Paul Kagame wamekutana Qatar kwa mazungumzo ya kwanza ya ana kwa ana tangu kuanza kwa mashambulizi ya Waasi wa M23, Januari 2025

Mkutano huo wa Machi 18, 2025 umefanyika wakati M23 wametangaza kujiondoa katika mazungumzo ya muafaka ambapo Viongozi wa Nchi hizo wamekubaliana kuhusu umuhimu wa kuendeleza majadiliano ili kuanzisha misingi imara ya amani ya kudumu

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na Qatar, DRC na Rwanda, Viongozi hao wamekubaliana juu ya kusitisha vita mara moja na bila masharti.

Ikumbukwe, DRC imekuwa ikiishutumu Rwanda kwa kutuma silaha na Wanajeshi kuunga mkono Kundi la M23, jambo ambalo Rwanda mara kwa mara imekuwa ikikanusha