Waendesha Mashtaka wameanza uchunguzi dhidi ya Rais wa zamani, Albero Fernandez (65) anayetuhumiwa kwa Unyanyasaji dhidi ya mke wake wa zamani Fabiola Yañez (43) ambaye amedai alilazimishwa kutoa Ujauzito na kupigwa.
Alberto ambaye alikuwa Rais wa Argentina mwaka 2019 hadi 2023, amekana kuhusika na tuhuma hizo na amepigwa marufuku kuondoka nchini humo.