Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump ametoa madai dhidi ya Rais Joe Biden kuwa aliwaagiza Majasusi wa FBI kumuua kwa Risasi walipovamia makazi yake na kufanya upekuzi ulioibua nyaraka za masuala ya Usalama wa Taifa nyumbani kwake.
Trump amesema “Biden aliagiza nguvu ya mauaji itumike katika uvamizi wa makazi yangu. Walipanga kunimaliza mimi pamoja na familia yangu, anafikiri kuwa anaweza kunitisha au kuniangusha”.
Ikumbukwe, Trump na Biden wanatarajiwa kukutana katika Uchaguzi Mkuu wa Marekani unaotarajiwa kufanyika Novemba 5, 2024 ambapo wachambuzi wanaeleza utakuwa na ushindani mkubwa kuliko Uchaguzi wa mwaka 2020.