Trump Atangaza Msimamo Mpya Kuhusu Putin, NATO na Ukraine

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

18 hours ago
rickmedia: trump-atangaza-msimamo-mpya-kuhusu-putin-nato-ukraine-354-rickmedia

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa licha ya kusikitishwa na mwenendo wa Rais wa Urusi, Vladimir Putin, katika mzozo unaoendelea wa Ukraine, bado hajaachana naye kabisa. Kauli hiyo imetolewa katika mahojiano ya kipekee kwa njia ya simu na BBC yaliyofanyika kutoka Ikulu ya White House.

Trump, ambaye hivi karibuni alitangaza msaada mpya wa silaha kwa Ukraine na kutishia kuiwekea Urusi ushuru wa hadi asilimia 100 endapo haitasaini makubaliano ya kusitisha mapigano ndani ya siku 50, alizungumza kwa hisia kuhusu uhusiano wake na Putin.

“Nimesononeshwa, lakini sijamalizana naye... Tumekuwa karibu kufikia makubaliano mara nne, lakini kila nikidhani tumekaribia, analipua jengo Kyiv,” alisema Trump.

Alipoulizwa ikiwa bado anamwamini kiongozi huyo wa Urusi, Trump alijibu kwa msimamo mkali:

“Siwezi kusema namwamini. Kwa kweli, mimi si mtu wa kuwaamini watu wengi. Hakuna ninayemuamini.”

Katika hatua ya kushangaza, Trump pia alibadilisha msimamo wake kuhusu Jumuiya ya Kujihami ya NATO, ambayo awali aliwahi kuiita “isiyo na maana.” Sasa anasema anaunga mkono juhudi za jumuiya hiyo, hasa baada ya mkutano wake na Katibu Mkuu mpya wa NATO, Mark Rutte.

“NATO si ya zamani tena. Inajitegemea kifedha sasa... Ninasimamia ulinzi wa pamoja kwa sababu inasaidia mataifa madogo kujilinda dhidi ya mataifa makubwa,” alieleza.

Kauli hizo zimetolewa wakati wa mahojiano maalum ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu jaribio la mauaji dhidi ya Trump katika mkutano wa kampeni huko Butler, Pennsylvania. Akizungumzia tukio hilo, Trump alisema:

“Sipendi kufikiria kama limenibadilisha. Kulifanyia tafakari kupita kiasi kunaweza kuwa na athari kubwa kisaikolojia.”

Trump pia alithibitisha kuwa anapanga kufanya ziara ya pili rasmi nchini Uingereza kama mgeni wa kifalme, ingawa tarehe rasmi bado haijatangazwa.