Loading...

Tundu Lissu adai Tume ya Uchaguzi sio huru,ni tume ya Urais

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 month ago
rickmedia: tundu-lissu-adai-tume-uchaguzi-sio-huruni-tume-urais-712-rickmedia

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Tundu Lissu amesema Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ni Taasisi isiyo Huru kwasababu Watendaji na Wateule wake Wanawajibika kwa Rais.

Amesema “Waangalizi wa Uchaguzi tangu mwaka 1995 wamesema hivyo, Mtendaji Mkuu, Wajumbe na Watumishi wake wote ni Wateule wa Rais na kwa mujibu wa #Katiba yetu, Watumishi hao wanafanya kazi kwa niaba ya Rais ambaye ni mamlaka yao ya nidhamu.”

Akizungumza kupitia Clouds FM, Lissu ameongeza kuwa “Kwa mujibu wa Katiba, Tume ina uwezo wa kutengeneza Majimbo ya Uchaguzi kwa ridhaa ya Rais, kwa maana nyingine ni kwamba Rais asipotoa ridhaa, Tume haina uwezo wa kutengeneza Majimbo ya Uchaguzi.”