Polisi Wamewakamata Wanachama 97 wa Kishia Kwa Mauaji ya Maafisa Polisi.
Jeshi la polisi nchini Nigeria linawashikilia wanachama 97 wa harakati za kiislamu nchini humo iliyopigwa marufuku katika nchi hiyo ambayo pia inajulikana kama Shia.
Wanachama hao wamezuiwa kufatia mapigano yaliyotokea jumapili mjini Abuja, awali mapigano hayo yalisababisha vifo vya polisi wawili na watatu kupata majeraha.
Pia ilifahamika kuwa magari matatu ya doria yalichomwa moto na Mashia wakati wa mapigano hayo.
Jeshi la Polisi la Nigeria linalaani vikali shambulio lisilosababishwa na wanachama wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN), inayojulikana kama kundi la Shia, dhidi ya maafisa wa polisi huko Abuja mnamo Agosti 25, 2024.