Loading...

Klau ya Yanga yafungiwa kufanya usajili (Kusajili)

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 month ago
rickmedia: klau-yanga-yafungiwa-kufanya-usajili-kusajili-393-rickmedia

Klabu ya Young Africans (YangaSC) imefungiwa kufanya usajili kwa kukiuka kanuni za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Uamuzi huo umefanywa na FIFA baada ya Klabu hiyo kukiuka Annexe 3 ya Kanuni ya Uhamisho wa Wachezaji (RSTP). Yanga haikuingiza uthibitisho wa malipo ya uhamisho wa Mchezaji katika Mfumo wa Usajili (TMS), licha ya kukumbushwa kufanya hivyo.

Kutokana na uamuzi huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nalo limeifungia Klabu ya Yanga kufanya usajili kwa Wachezaji wa ndani.