Kiungo wa Manchester City, Matheus Nunes, anatuhumiwa kwa kukwapua simu ya shabiki ambaye alitaka kumpiga picha, wakati walipokutana msalani kwenye ukumbi wa starehe usiku.
Licha ya taarifa hizo kujulikana leo Oktoba 2, 2024, Nunes (26) raia wa Ureno ambaye alisajiliwa na City kwa Pauni Milioni 53 (Tsh. Bilioni 192.4) akitokea Wolves Mwaka 2023, inadaiwa alishikiliwa Septemba 8, 2024 kisha kupelekwa Kituo cha Polisi kuhojiwa.
Imeelezwa Nunes aliichukua simu na hakuirudisha, Askari Polisi walipofika walimfunga pingu na kuondoka naye, aliachiwa saa kadhaa baadaye baada ya Wakili wake kufika na suala hilo linatarajiwa kutolewa maamuzi Mahakamani.