Sare ya 1-1 yawatoa kinyonge Uwanjani Mashabiki wa Simba Sports Club

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 year ago
rickmedia: sare-1-1-yawatoa-kinyonge-uwanjani-mashabiki-simba-sports-club-704-rickmedia

Goli la kusawazisha la Serge Pokou wa 'ASECMimosas' ya Nchini  'Ivory Coast', limesababisha mashabiki wa 'Simba Sports Club'  watoke Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam wakiwa wanyonge baada ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika Kundi B kumalizika kwa sare ya 1-1.

Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ alianza kufunga upande wa Simba kwa njia ya penati lakini wageni waliamka kipindi cha pili na kutoa ushindani mkali na kusawazisha goli.

Mchezo ujao ni Desemba 2, 2023, Simba itakuwa ugenini Nchini Botswana kucheza dhidi ya 'JwanengGalaxy' wakati 'ASEC' itaikaribisha 'Wydad' ya Nchini Morocco.