Simba yaingia robo fainali kwa kishindo, yafunga 6-0

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 year ago
rickmedia: simba-yaingia-robo-fainali-kwa-kishindo-yafunga-6-0-335-rickmedia

Timu ya Simba imemaliza Hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kupata ushindi mnono wa magoli 6-0 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Waliocheka na nyavu katika mchezo huo ni Saidi Ntibazonkiza (7), Pa Omary Jobe (14), Kibu Denis (22), Clatous Chama (76), Ladaki Chasambi (86) na Fabrice Ngoma (89).

Baada ya matokeo hayo, msimamo wa mwisho wa Kundi B, ASEC Mimosas ya Ivory Coast imeongoza kwa kuwa na pointi 11, Simba ina 9 sawa na Wydad AC ya Morocco huku Jwaneng ikiwa na alama 4.

Hii inakuwa mara ya kwanza kwa Tanzania kuingiza timu mbili Hatua ya Robo Fainali ambazo ni Simba na Yanga.