Msanii Mkongwe wa muziki kutoka kundi la #WakaliKwanza #QJ ameripotiwa kuokoka tena kwa mara nyingine baada ya kuokoka Mwaka 2010 na badae kudaiwa kurudi kwenye matumizi ya Pombe Mwaka 2015.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa Pastor #Kabigumila amethibitisha hilo.
KUNDI LA BONGO FLEVA WAKALI KWANZA
MWAKA 2004 HADI 2009
Kundi hili liliundwa na vijana watatu wenye vipaji vikubwa vya kuimba Joslin, Makamua na QJ,
Walifanya hit song nyingi za muziki huo na kubwa kuliko zote ilikuwa NATAMANI,
Kwenye wimbo huu kijana aitwaye JOSEPH KELVIN MAPUNDA A.K.A QJ anaimba ubeti huu chini;
Mtoto anang'ara kama candle light,
Ana face nzuri ya Kiafrika,Killer boy, Kenya boy, MJ wanamjuaaaa,Uzuri wake hafanani na waridi ama ua poriiiii poriii,
Huyu QJ mwenye mashairi haya na SAUTI YA AJABU YA KUSISIMUA, aliokoka mwaka 2010 kanisa la TFC chini ya Askofu Malasi, akasimama, lakini mwaka 2015 aliondoka na kwa kukosa malezi sahihi ya kiroho akaanza tena ULEVI WA POMBE,
Wiki iliyopita Mungu alinisukuma kutafuta namba yake hadi nikaipata, na kumbe alisharudi kwao kijijini huko wilaya ya Mbinga kwa mama yake, lakini akiwa bado anasumbuka na kunywa japo si kwa kasi ile ya mwanzo!
Nikampata kwa simu, nikaongea naye na kumtumia nauli aje Dar, kwa ruhusa ya mama yake na baba yake mdogo JUMAPILI HII ILIYOPITA YA 01.09.2024 AKAFIKA NA AKAFUNGULIWA UPYA, NA MUNGU AKANIAGIZA NIMLEE AWE MCHUNGAJI AMTUMIE KUVUNA KIZAZI HIKI CHA BONGO FLEVA NA WALIONASWA KWENYE WAVU WA MUZIKI WA KIDUNIA!
Nimepewa baraka na wazazi wake,
Na sasa ninaye ABC GLOBAL DEPO (MAHALI PA SHULE YA HUDUMA), ameanza tayari kuchongwa kuwa CHOMBO CHA MUNGU CHA MAVUNO MAKUU MUDA MCHACHE UJAO,
Usiache kumuombea ili alete majibu kwenye kizazi hiki, na kumvunia Bwana Yesu mavuno kwa sauti na kipawa chake baada ya malezi haya,
Natanguliza picha, lakini VIDEO YOTE YA TUKIO HILI INA UPLOAD UTAIONA HAPA,