Kwa mujibu wa gazeti la New York Times, siku moja tu baada ya kuwasilisha malalamiko yake, mwimbaji wa R&B Cassie amefikia suluhu katika kesi yake dhidi ya Diddy, akimtuhumu kwa ubakaji na unyanyasaji wa miaka mingi.
Katika taarifa, #Cassie alielezea nia yake ya kutatua suala hilo kwa amani na alishukuru familia yake, mashabiki, na wanasheria kwa msaada wao. #Diddy pia alitoa taarifa fupi akimtakia kila la heri #Cassie na familia yake. Masharti ya suluhu hayakufichuliwa, lakini inamaanisha kuwa hakutakuwa na kesi.