Ikiwa leo Rais Samia Suluh Hassan amefanya tafrija Ikulu ya Jijini Dar Es Saalam katika kusheherekea Miaka yake mitatu ya kukaa madarakani alialika baadhi ya wasanii ili kujumuika naye, Diamond Platnumz na Harmonize ni miongoni mwa wasanii hao na wawili hao wamekutana na kupeana mikono baada ya kukutana Ikulu.
Ikumbukwe Harmonize alisema kuwa atampiga simu Diamond ili wamalize tofauti zao lakini kabla ya mambo kuanzia kwenye simu wawili hao wamekutana Ikulu.
Kwenye mazungumzo yao #Harmonize anasikika akimwambia #Diamondplatnumz kuwa atampigia siku ya kesho apokee simu. Diamond anamjibu kuwa nimebadilisha namba.