Wapenzi wa teknolojia na mitindo ya kisasa walikusanyika kwa shangwe kubwa katika jiji la Dodoma kushuhudia tukio la kihistoria uzinduzi rasmi wa oraimo shop, duka la kwanza la aina yake kwa mkoa wa kati linalouza bidhaa rasmi za oraimo, watengenezaji mashuhuri wa vifaa vya kisasa vya teknolojia barani Afrika.
Katika tukio hilo la kuvutia lililohudhuriwa na mashabiki na wateja wa oraimo pia ilitambulisha rasmi bidhaa yake mpya iliyosubiriwa kwa hamu oraimo Watch 5 Lite. Saa hii mpya ya kisasa inakuja na muundo maridadi, uwezo wa kupiga simu, kufuatilia afya, mazoezi, na betri inayodumu hadi siku 7 bila kuchaji. Ni sukuhisho kamili wa teknolojia na mitindo.
Meneja wa Mauzo wa oraimo Tanzania, aliwaeleza waandishi wa habari kuwa uzinduzi wa duka hilo ni sehemu ya mkakati wa kampuni wa kusogeza bidhaa bora karibu zaidi na watumiaji. "Dodoma ni kitovu cha maendeleo nchini, na tunataka kuhakikisha kila Mtanzania anapata fursa ya kufurahia bidhaa zetu kwa urahisi, uhakika na huduma bora zaidi."
Wateja waliohudhuria walipata fursa ya kuona, kujaribu na kununua bidhaa kwa punguzo maalum, pamoja na kujinyakulia zawadi mbalimbali kutoka oraimo. Tukio hilo lilifanyika katika hali ya furaha, muziki na burudani ya kipekee.
Kwa sasa, wakazi wa Dodoma na mikoa jirani wanaweza kufurahia urahisi wa kupata bidhaa halisi (original) za oraimo zikiwemo power banks, earbuds, smartwatches, na vifaa vingine vya teknolojia kwa huduma ya kitaalamu na dhamana kamili.