Dj Mushizo Aandika Ujumbe kwa Mara ya Kwanza Tangu Apate Ajali ya Moto

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 hour ago
rickmedia: mushizo-aandika-ujumbe-kwa-mara-kwanza-tangu-apate-ajali-moto-575-rickmedia

Kwa mara ya kwanza tangu apate ajali mbaya ya moto nyumbani kwake, mtayarishaji maarufu wa muziki na DJ, Dj Mushizo, ameibuka hadharani na kuandika ujumbe wa kugusa moyo kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram.

Katika ujumbe huo, Dj Mushizo amefunguka kuhusu safari yake ya uponyaji na changamoto alizopitia tangu alipopatwa na tukio hilo baya. Akiambatanisha maneno hayo na pich“ALHAMDULILAH 🙏🏾, Kila jeraha lina hadithi yake na yangu ni ya mapambano na matumaini. Si mwisho, bali mwanzo mpya.”

Amekiri kuwa kipindi cha kuuguza majeraha yake kilikuwa kigumu sana, na mara kadhaa alikata tamaa ya maisha kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapitia. Hata hivyo, anasema hakukata tamaa kabisa kwani kulikuwa na sababu ya kuendelea kupigana.

“Kulikuwa na siku ambazo nilijihisi kukata tamaa ya maisha, siku ambazo nilijiuliza kama ningeweza kuendelea kuishi. Lakini, nilikuwa na sababu ya kuendelea – kwakuwa upendo wa wale walionizunguka, imani yangu kwa Mungu, na azma yangu ya kuishi maisha kamili.”

Ujumbe huo umetoka kama alama ya shukrani kwa wote waliomwombea na kumpa moyo wakati wa kipindi kigumu. Amemaliza kwa kusema:

“ASANTENI WOTE – HAKIKA MUNGU AMEJIBU MAOMBI YETU.”

Miezi kadhaa iliyopita, taarifa zilisambaa kuhusu tukio la kuungua kwa Dj Mushizo akiwa nyumbani kwake. Iliripotiwa kuwa alikumbwa na ajali ya moto iliyosababisha majeraha makubwa mwilini mwake. Tangu wakati huo, amekuwa kimya mitandaoni na alipotea kwenye macho ya umma huku akiendelea na matibabu.

Mashabiki wake na wadau wa burudani wameendelea kuonyesha mshikamano na upendo, wakimtumia salamu za faraja na kumuombea apone haraka.