Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro amefanya mabadiliko ya Kamati ya Tuzo za Muziki na kufanya uteuzi wa Wajumbe wataohusika katika kuratibu Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) kwa mwaka 2023-2024.
Kamati hii inaongozwa na David Minja ambaye ni Mwenyekiti, Christine Mosha (Seven) Makamu Mwenyekiti, Mrisho M.Mrisho Katibu na Wajumbe ambao ni P Funk Majani Mtayarishaji wa Muziki, Chris Torline na Natasha Stambuli.
Akiizungumzia kamati hiyo, Katibu Mtendaji wa #BASATA, Dkt. Kedmon Mapana amesema, “Timu hii ina weledi na ubobevu na iko tayari kuinua Tuzo za Muziki kwa viwango vipya, kwa ujuzi wao usio na kifani na mtazamo wao wa kipekee, watarekebisha tasnia ya muziki na kukuletea TMA ambayo haijawahi tokea”.
Mabadiliko hayo yanafanywa ikiwa ni baada ya Wadau wa Muziki kuwa na maoni ya kutaka Tuzo hizo zifanyiwe maboresho ikiwemo Kamati zinazohusika na zoezi zima kuwa na uzoefu katika masuala ya Muziki.