Rapa na muigizaji LL Cool J, mwenye umri wa miaka 56, amerudi na albamu yake mpya baada ya zaidi ya. miaka 10. Akihojiwa na Variety, LL Cool J alielezea nia yake ya kubadili mtazamo wa hip-hop kuhusu umri, akisema kuwa watu hawakumuelewa alipoeleza kuwa anataka kurekodi albamu ya kisasa. Albamu yake mpya The Force, iliyotayarishwa na Q-Tip, ni ya kwanza tangu Authentic ya 2013.
LL Cool J alieleza kwamba muziki wake unalenga kudhihirisha kuwa wasanii wakongwe bado wanaweza kuwa na umuhimu kwenye hip-hop, ambayo mara nyingi inaonekana kuwa ya vijana.
Katika mahojiano hayo, alifichua pia kuwa ana muziki ambao haujaachiliwa alioufanya na #MichaelJackson, na kwamba Michael alimuonyesha upendo na heshima kubwa.
"Michael Jackson kwangu ni mfalme," alisema #LLCoolJ, akieleza kuwa bado ni shabiki mkubwa wa mwimbaji huyo maarufu.