Rushaynah Afunguka Kuhusu Mahusiano yake na Harmonize, Aweka wazi ukweli wote

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

2 years ago
rickmedia: rushaynah-afunguka-kuhusu-mahusiano-yake-harmonize-aweka-wazi-ukweli-wote-283-rickmedia

Aliyekuwa mke wa Haji Manara, Rushaynah ambaye waliachana miezi kadhaa iliyopita kwa kupewa talaka na mumewe, Leo amekuja na usemi juu ya kile kinachoendelea katika mitandao ya kijamii juu ya video zinazosambaa Kati yake na msanii wa muziki Tanzania, Harmonize ambazo zimesambaa siku chache zilizopita zikiwaonyesha wawili wakiwa pamoja katika maeneo mbalimbali.

Video hizo zimewafanya baadhi ya watu kuamini Harmonize na Rushaynah wanatoka kimapenzi ikumbukwe miezi kadhaa iliyopita baada ya Haji Manara kuachana na Rushaynah kuna video ilosambaa kimuonyesha Rushaynah akiwa nyumbani kwa Harmonize.

Kutokana na mitazamo ya watu juu ya kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii, Rushaynah ametoka hadharani kupitia ukurasa wake wa Instagram Kwa kusema

" Mimi Rushaynah Kwa kutambua kinachoendea mitandaoni kwenye page mbalimbali za udaku,ningependa kuweka Sawa ili kila mtu ajue hizo video zinazosambaa zikinionyesha Mimi nikiwa na Rajabu ilikuwa ni Katika siku ya kuzindua wimbo wake (pool party) yote yaliyofanyika/niliyofanya ni Kwajili ya kushow love katika kazi zake.

Naomba isitafsiriwe vinginevyo na kuleta habari hasi dhidi yangu, hatuna mahusiano ya kimapenzi kama ambavyo inaripotiwa na baadhi ya pages, Sisi ni marafiki tu, Ahsanteni."

Party ambayo ilifanyika kwa Harmonize ilikuwa inaambatana na uzinduzi wa wimbo wake akimshirikisha Ruger msanii kutoka Nigeria ambao ni Single Again Remix.



(Imeandaliwa na Kanubo)