Shahidi ajitoa kwenye kesi ya Diddy ya unyanyasaji

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

4 months ago
rickmedia: shahidi-ajitoa-kwenye-kesi-diddy-unyanyasaji-550-rickmedia

Kalenna Harper, aliyewahi kuwa mwanachama wa kundi la Diddy-Dirty Money, amejitenga na kesi ya Dawn Richards dhidi ya Sean "Diddy" Combs.

Kwenye taarifa yake iliyotolewa Ijumaa, Harper alisema hajawahi kushuhudia vitendo vya unyanyasaji dhidi ya mpenzi wa zamani wa Diddy, Cassie Ventura, wala tabia yoyote isiyo ya kisheria. Alisema, "Madai mengi yaliyopo kwenye kesi hii hayawakilishi uzoefu wangu, na mengine hayaendani na ukweli wangu."

Richards alimfungulia Diddy kesi wiki hii, akimshutumu kwa unyanyasaji wa kijinsia na mateso yasiyo ya kibinadamu, akidai kuwa yeye na wengine walishuhudia Diddy akimnyanyasa Cassie. Diddy amekanusha madai hayo kupitia wakili wake.