Madaktari nchini India wamejikuta wakipigwa na butwaa baada ya kukuta funguo, mashine za kukata kucha, na hata kisu kutoka tumboni mwa kijana, aliyeripotiwa kuwa na umri wa miaka ishirini.
Suala hilo lilikuja kujulikana baada ya mama wa mgonjwa ambaye hakutajwa jina kugundua kwamba funguo za kabati lake la nguo hazioni na kumuuliza mtoto wake na kujibiwa kuwa amezimeza ambapo mwanzo jibu hilo lilichukuliwa kama utani.
Aligundua kuwa hakuwa akidanganya baada ya kumsafirisha hadi hospitali ya Motihari, Bihar, ambapo uchunguzi wa ultrasound ulionyesha kwamba alikuwa amemeza funguo pamoja na vitu vingine visivyoweza kuliwa.
Wakati wa operesheni iliyofuata, daktari-mpasuaji msimamizi Dk. Kumar na timu yake pia walichomoa vikata kucha na kisu cha kukunja.Licha ya ugumu wa upasuaji huo, mgonjwa huyo anaripotiwa kupata nafuu.
Dk. Kumar aliunga mkono nadharia yake, akidai kwamba vitendo vya mvulana huyo viliathiriwa na utumiaji wake mwingi wa simu (Smartphone) na ugonjwa wa akili.