Afande Fatma afika Mahakamani , Kesi yake ya ahirishwa

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

4 months ago
rickmedia: afande-fatma-afika-mahakamani-kesi-yake-ahirishwa-74-rickmedia

Kesi iliyofunguliwa na Paul Kisabo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma dhidi ya Afande Fatma Kigondo ilishindwa kusikilizwa Agosti 23, 2024 baada ya afande huyo kutotokea Mahakamani.

Uamuzi wa kumpatia hati ya wito kwa mara nyingine ulitolewa na Hakimu Mkazi wa Dodoma, Francis Kishenyi ambaye alikuwa anaisikiliza kesi hiyo.

Aidha, Paul Kisabo akizungumza na Waandishi wa Habari Septemba 5, 2024 amesema kuwa Kesi ya Fatma imehairishwa hadi Oktoba 7, 2024 baada ya Hakimu Kishenyi kuhamishwa Kituo cha Kazi, akisisitiza kuwa kwa sasa kesi hiyo bado haijapangiwa Hakimu mwingine wa kuisikiliza.