Aliyekuwa Balozi wa Baba Mtakatifu katika nchi mbalimbali duniani, Mtanzania Askofu Mkuu Novatus Rugambwa amefariki dunia usiku wa Septemba 16, 2025 mjini Roma, Italia.
Askofu Mkuu Rugambwa alizaliwa Oktoba 8, 1957 mkoani Kagera na kuwekwa wakfu Upadre Julai 6, 1986 na Askofu Nestorius Timanywa wa Jimbo Katoliki Bukoba. Machi 18, 2010 aliwekwa wakfu Uaskofu na Kardinali Tarcisio Bertone, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Vatican.
Marehemu aliwahi kuhudumu kama Balozi wa Baba Mtakatifu katika nchi mbalimbali zikiwemo Angola, Honduras na Visiwa vya Fiji.