Septemba 15, 2025, katika Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro, limefunguliwa shauri la Uhujumu Uchumi namba 22415/2025 dhidi ya aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji cha Ruvu Remiti, Godbless Felix Mollel.
Mshtakiwa anadaiwa kufanya ubadhirifu wa shilingi milioni 3.3 za kijiji kinyume na sheria za Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Kanuni za Adhabu. Mwendesha mashtaka wa TAKUKURU, Faustin Mushi, alisoma mashtaka hayo, huku mshtakiwa akikataa makosa yote.
Kesi imeahirishwa hadi Septemba 25, 2025 kwa ajili ya kusikilizwa hoja za awali.
Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya wadhamini wawili walioweka bondi ya shilingi milioni 2 kila mmoja.