Mahakama Kuu ya Afrika Kusini imetupilia mbali rufaa ya familia ya aliyekuwa Rais wa Zambia, Edgar Lungu, iliyotaka kusitisha urejeshaji wa mwili wake Zambia kwa mazishi ya kitaifa.
Familia hiyo, iliyokuwa na nia ya kupeleka shauri hilo Mahakama ya Rufaa ya Juu (SCA), imeamriwa pia kulipa gharama za kesi.