Bilionea na Mfanyabiashara Mustafa Rajabali Jaffer (Sabodo) amefariki leo Machi 23, 2024 akiwa Nyumbani kwake Masaki.
Danstan ambaye ni Mtoto wa Sabodo amenukuliwa na Daily News Digital akisema taratibu za mazishi zinaendelea na maziko yatafanyika katika Makaburi ya Mtaa wa Bibi Titi Mohamedi karibu na CBE.
Sabodo, Mzaliwa wa Lindi alifanya Biashara katika Nchi za Kenya, Ufaransa, India, Sudan na Zimbabwe, alikuwa akichangia Miradi ya Maendeleo ya Huduma za Jamii pamoja na uimarishaji wa Demokrasia.
Aliwahi kuchangia Fedha kwa nyakati tofauti kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama Cha Mapinduzi (CCM).