Mamlaka inayosimamia Huduma za Umeme (Kenya Power PLC) imetangaza tatizo la kukosekana kwa Nishati hiyo katika maeneo kadhaa ya Nchi.
Taarifa ya leo Septemba 6, 2024 imeeleza kuwa maeneo ambayo hayajaathirika na hitilafu hiyo ni Kaunti zilizopo Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Magharibi mwa Nchi.
Hitilafu hii inakuja ikiwa ni Wiki moja tangu Kenya iliporipoti tatizo la kukatika tena kwa Umeme, ambapo sehemu kubwa ya nchi iliathirika isipokuwa maeneo ya Kaskazini na Magharibi.