Watu 11 wamepoteza maisha na wengine 44 kujeruhiwa baada ya Basi la Abiria la A-N Coach (T282 CXT) lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Tabora, kupinduka wakati likikwepa Lori na kuingia mtaroni.
Kamanda msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, Wilbert Siwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo Septemba 6, 2024.
Aidha, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Chunya, Darson Andrew amethibitisha idadi ya vifo huku akieleza kati ya majeruhi 44, wanne wana hali mbaya na watapewa rufaa kupelekwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.