Ndugu wawili wamekutwa na hatia ya kumdanganya Jordan DeMay kwa mmoja wao kujifanya Msichana kupitia Instagram na kumshawishi atume picha za faragha na kuanza kumtisha kuwa watazisambaza kama hatawapa Fedha.
Imeelezwa, Jordan aliwalipa Fedha hadi alipoishiwa na kuwaambia Washtakiwa angejiua endapo wangevujisha picha hizo ambapo walimjibu "Vizuri, fanya haraka kabla hatujakufanya ufanye hivyo". Jordan alijiua muda mchache baada ya kuwasiliana nao.
Aidha, Samuel na Samson wenye Miaka 24 na 21 wanatajwa kuwafanyia vitendo vya aina hiyo Watu wengine 38, huku 13 kati yao wakiwa wenye Umri chini ya Miaka 18.