Shahidi mmoja asikilizwa Kesi ya Binti aliyebakwa Yombo

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

9 months ago
rickmedia: shahidi-mmoja-asikilizwa-kesi-binti-aliyebakwa-yombo-919-rickmedia

Wakili wa upande wa utetezi Meshack Ngamando, wa kesi ya ubakaji na ulawiti wa”Binti wa Yombo” amesema kesi hiyo imeendelea Agosti 20, 2024 kwa kusikilizwa shahidi mmoja kati wa watano kutokana na muda.

Wakili Ngamando amesema “Kesi inasikilizwa vizuri na hakuna shida yoyote, Wananchi tuwe na utulivu tusikilize kesi nina imani kwamba haki itatendeka.”

Watuhumiwa Wanne wa kesi hiyo walirudishwa rumande mara baada ya kesi kuahirishwa, itaendelea Leo Agosti 21, 2024, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma.