Loading...

Waandamanaji zaidi ya 200 wakamatwa kwa kupinga mapendekezo ya ongezeko la kodi

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

4 weeks ago
rickmedia: waandamanaji-zaidi-200-wakamatwa-kwa-kupinga-mapendekezo-ongezeko-kodi-266-rickmedia

Waandamanaji zaidi ya 200 wamekamatwa katika Mji wa Nairobi kutokana na Maandamano ya Wananchi wanaopinga ongezeko la Kodi zilizopendekezwa katika Muswada wa Fedha ambao unatarajiwa kuwasilishwa Bungeni.

Mashirika ya Kiraia yanasema licha ya kukamatwa kwa Watu hao, lakini mchakato wa Maandamano na mpango wa kukaa nje ya Jengo la Bunge utaendelea kama walivyopanga.

Baadhi ya mapendekezo ya Kodi katika Muswada huo yameshaondolewa baada ya mkutano uliofanyika Juni 18, 2024 kati ya Wabunge wa Chama tawala na Rais William Ruto ikiwemo kodi ya VAT ya 16% kwenye Mkate na kodi ya 2.5% ya kila Mwaka kwenye Magari ambayo ilikuwa iwekwe kwenye Bima.

Wabunge wanatarajiwa kujadili Muswada huo kuanzia leo Jumatano (Juni 19, 2024) na zoezi la kupiga kura limepangwa kufanyika Jumatatu.