Zaidi ya watu 670 wahofiwa kufariki kwenye maporomoko ya udongo huko Papua New Guinea

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 year ago
rickmedia: zaidi-watu-670-wahofiwa-kufariki-kwenye-maporomoko-udongo-huko-papua-new-guinea-50-rickmedia

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wahamiaji (IOM) limesema zaidi ya Watu 670 wanaweza kuwa wamefariki baada ya kutokea maporomoko ya Udongo katika Vijiji vya Yambali na Enga nchini humo.

Mkuu wa Shirika hilo, Serhan Aktoprak amesema idadi inazidi kuongezeka kutokana makadirio ya idadi ya nyumba zilizofunikwa na Vifusi kuzidi 150 katika eneo la vijiji viwili.

Kwa mujibu wa waokoaji, kazi ya kutafuta waliofariki na manusura inakuwa ngumu kutokana na wingi wa Udongo uliofunika maneno mengi yenye Mawe makubwa pamoja na kasi kubwa ya Maji.