Ghana Yapitisha Sheria Ngumu Ya Jela Kwa Watakao Jihusisha na Mapenzi Ya Jinsia Moja

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 year ago
rickmedia: ghana-yapitisha-sheria-ngumu-jela-kwa-watakao-jihusisha-mapenzi-jinsia-moja-22-rickmedia

Bunge la Ghana limepitisha mswada mpya mgumu unaoweka kifungo cha hadi miaka mitatu jela kwa yeyote atakayepatikana na hatia ya kujitambulisha kama LGBTQ+.

Pia inaweka kifungo cha juu zaidi cha miaka mitano jela kwa kuunda au kufadhili vikundi vya LGBTQ+.

Wabunge walipuuza majaribio ya kubadilisha vifungo vya jela na huduma za jamii na ushauri nasaha.

Ni ishara ya hivi punde ya kuongezeka kwa upinzani dhidi ya haki za LGBTQ+ katika taifa hilo la kihafidhina la Afrika Magharibi.

Mswada huo, ambao uliungwa mkono na vyama viwili vikuu vya kisiasa vya Ghana, utaanza kutekelezwa iwapo tu Rais Nana Akufo-Addo atautia saini kuwa sheria.

Hapo awali alisema kuwa atafanya hivyo ikiwa raia wengi wa Ghana watamtaka.

Mapenzi ya jinsia moja tayari ni kinyume cha sheria nchini Ghana - ina adhabu ya miaka mitatu jela.

Mwezi uliopita Amnesty International ilionya kuwa mswada huo unaleta vitisho kwa haki za kimsingi na uhuru wa watu wa LGBTQ+.