Haiti yaunda Baraza la mpito, uchaguzi kufanyika February 2026

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

8 months ago
rickmedia: haiti-yaunda-baraza-mpito-uchaguzi-kufanyika-february-2026-896-rickmedia

Haiti imetangaza kuundwa kwa Baraza la Mpito lenye jukumu la kurejesha hali ya utulivu kufuatia ghasia zilizozuka kutoka kwa Magenge ya Uhalifu kulikosababisha Waziri Mkuu, Ariel Henry, kutangaza kujiuzulu Mwezi mmoja uliopita.

Baraza lina jukumu la kuteua Waziri Mkuu mpya na Serikali kwa haraka kwa kuzingatia sera mbalimbali za Siasa ya Haiti. Pia, Kuundwa kwa Baraza hilo linaloungwa mkono na Marekani ni hatua ya kuelekea kufanyika Uchaguzi wa Rais ifikapo Februari 2026.

Nchi hiyo haijafanya Uchaguzi tangu 2016 na imekuwa bila Rais tangu Jovenel Moise alipouawa Mwaka 2021.