Bunge la India limepitisha Muswada wa Uendelezaji na Udhibiti wa Michezo ya Mtandaoni, 2025, unaopiga marufuku kabisa michezo ya mtandaoni ya kubashiri kwa pesa halisi (real-money games), iwe ya bahati nasibu au ujuzi.
Benki na taasisi za kifedha zimezuiwa kushughulikia miamala ya michezo hiyo na Adhabu ya kifungo hadi miaka 3 au faini ya hadi &10m ($115,000).
Mbali na hivyo Wasanii watakaotangaza michezo hiyo wanaweza kufungwa hadi miaka 2 au kutozwa faini ya ?5m ($57,000).
Serikali imesema hatua hii inalenga kulinda jamii kufuatia visa vya watu kujitoa uhai baada ya kupoteza fedha kwenye michezo hiyo.
Hata hivyo, wadau wa sekta wanasema sheria hii inaweza kuua kampuni halali za ndani na kuacha nafasi zaidi kwa majukwaa haramu ya nje ya nchi, na huenda ikapinga Katiba ya India (Ibara 19(1)(g)) inayolinda haki ya kufanya biashara.