Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei ametoa wito wa umoja wa kitaifa akisema Marekani inajaribu kuiyumbisha Jamhuri ya Kiislamu.
Akihutubia katika msikiti mjini Tehran, Khamenei alisema maafisa wa Marekani walikutana Ulaya kujadili mustakabali wa Iran baada ya kuuangusha utawala uliopo. Amesisitiza kuwa Iran imeungana na tayari ilishinda vita vya siku 12 dhidi ya Israel mwezi Juni, lakini akaonya kuhusu migawanyiko ya ndani inayochochewa na mataifa ya kigeni.