Muhammad Yunus (84) ataongoza Serikali ya Mpito ya Bangladesh baada ya Waziri Mkuu wa zamani Sheikh Hasina, kujiuzulu na kukimbia Nchi kufuatia vuguvugu kubwa la kupinga utawala wake lililoongozwa na Wanafunzi.
Viongozi wa Maandamano ya Wanafunzi, Makamanda wa Majeshi, Wanachama wa Jumuiya za Kiraia, pamoja na baadhi ya Viongozi wa Jumuiya za Wafanyabiashara, walifanya Mkutano na Rais kwa zaidi ya Saa 5, Usiku wa Agosti 6, 2024 ili kumchagua Mkuu wa Serikali ya Mpito.
Yunus alitunukiwa ‘Nobel Prize’ Mwaka 2008 kwa kuwa Muasisi wa Mikopo Midogo Nchini humo, ambapo Mwaka 1983 alianzisha Benki ya Grameen ili kutoa Mikopo Midogo kwa Wajasiriamali ambao hawakuwa na Vigezo vya kupata Mikopo ya Kawaida, hatua iliyosaidia kupunguza Umasikini Nchini Bangladesh.