Wafungwa 4,068 kutoka katika magereza mbalimbali nchini Nigeria wameachiwa Huru

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

2 weeks ago
rickmedia: wafungwa-4068-kutoka-katika-magereza-mbalimbali-nchini-nigeria-wameachiwa-huru-971-rickmedia

Serikali ya Nigeria imewaachia huru Leo November 20,2023 Takribani wafungwa 4,068 kutoka katika magereza mbalimbali nchini Humo hususa ni kwa wale walioshindwa kulipa faini

Pia huu ni mpango wa nchi ya Nigeria katika kuhakikisha kwamba wanapunguza msongamano wa watuhumiwa wengi kwenye magereza nchini humo

Aidha, waziri wa mambo ya ndani, mhe; Olubunmi Tunji -ojo Alisema "kabla ya msamaha huo kutolewa hapo mwanzo tulikuwa na wafungwa 80,804 kwenye magereza 253 na changamoto ni kwamba tunashindwa kuwahudumia wafungwa wote ndio maaana serikali imeamua kufanya maamuzi ya kuwaachia huru baadhi ya wafungwa"

Kwa hivi karibuni Takwimu zilizofanywa na Umoja wa Mataifa (UN) zimebaini wazi kwamba Nigeria Ina wafungwa wengi sana na hata hivyo wanashindwa kuwahudumia.


(Imeandaliwa na Halfan Mkalinga)