Waziri Mkuu Sheikh Hasina ameripotiwa kujiuzulu na kuondoka katika Mji Mkuu (Dhaka) wakati kukiwa na maandamano makali ya kumtaka ajiuzulu.
Uamuzi huo umekuja ikiwa ni muda mfupi tangu Umoja wa Mataifa uitake Serikali kusitisha mara moja machafuko yanayoendelea Nchini humo ambayo yamesababisha vifo vya takriban watu 200, wakiwemo Maafisa wa Polisi.