Cristian Ronaldo awa mtu wa kwanza Duniano kufikisha Magoli 900 kwenye Mechi zote alizocheza

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

4 months ago
rickmedia: cristian-ronaldo-awa-mtu-kwanza-duniano-kufikisha-magoli-900-kwenye-mechi-zote-377-rickmedia

Nyota wa Soka kutoka Ureno, Cristiano Ronaldo, ameweka rekodi ya kuwa Mchezaji wa kwanza Duniani kufikisha Magoli 900 katika maisha yake ya Soka, rekodi ambayo ni kwa mujibu wa Tovuti ya Transfermarkt.

Akiichezea Ureno katika mchezo dhidi ya Croatia, Ronaldo amefunga Goli hilo katika dakika ya 34 baada ya Diogo Dalot kufunga goli la utangulizi, ingawa baadaye (Dalot) alijifunga na kusababisha mchezo kumalizika kwa Magoli 2-1.

Kufuatia ushindi huo dhidi ya Croatia, Ureno ilifungana pointi na Poland inayoongoza Kundi A1 ambayo iliichapa Scotland mabao 3-2 katika Mchezo wa UEFA Nations League.